• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asisitiza kuimarisha uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Nigeria

    (GMT+08:00) 2014-05-08 10:21:53

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alifanya mazungumzo na rais Goodluck Jonathan wa Nigeria mjini Abuja kuhimiza kuongeza ushirikiano kati ya zao.

    Bw Li amesema kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kunawanufaisha watu wa pande mbili, kunachangia maendeleo na ustawi wa kikanda na wa dunia nzima. Pia amesema China inapenda kupanua ushirikiano na Nigeria katika biashara na uwekezaji, kuhimiza uwiano wa biashara, na kuimarisha ushirikiano katika ujenzi wa miundo mbinu, kilimo, nishati na safari za anga ya juu.

    Rais Jonathan amesema Nigeria inaishukuru China kwa kutoa misaada na kuunga mkono nchi yake, nchi za Afrika na Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS. Amesema Nigeria inapongeza utaratibu wa ushirikiano kati ya Afrika na China uliotajwa kwenye hotuba aliyoitoa Bw. Li Keqiang kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika ambao utachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Afrika, na inapenda kuhimiza ushirikiano na China katika sekta za reli, safari za anga ya juu, reli nyepesi, biashara, uwekezaji, kilimo, maji na umeme na nishati. Amesema Nigeria inazikaribisha kampuni za China kuwekeza zaidi nchini Nigeria, na upande wa Nigeria utaandaa mazingira mazuri kwa wawekezaji wa China.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako