• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China atoa hotuba kwenye mkutano wa kilele wa Afrika wa Baraza la uchumi la dunia

    (GMT+08:00) 2014-05-08 22:02:15


    Mheshimiwa rais Goodluck Jonathan,

    Waheshimiwa marais na wakuu na serikali mnaohudhuria mkutano huu,

    Mabibi na mabwana,

    Nafurahi ujumbe wa serikali ya China ambao si nchi ya Afrika kuhudhuria pamoja nami kwenye mkutano wa kilele wa Afrika wa Baraza la uchumi la dunia. Namshukuru Bw. Klaus Schwab kwa kunialika, na namshukuru rais Jonathan kwa mapokezi mazuri. Kauli mbiu ya mkutano huu ni "Kufaidika na ongezeko la uchumi kwa haki na usawa, na kuleta nafasi za ajira", ambayo inaendana na hali halisi na ina mvuto mkubwa. Kwa niaba ya serikali ya China, napenda kutoa pongezi kwa kufunguliwa kwa mkutano huu!

    Bara la Afrika ni chanzo muhimu cha ustaarabu wa binadamu. Katika miaka mia moja iliyopita, mabadiliko makubwa yametokea kwenye bara hili la kale lenye miujiza. Watu wa nchi za Afrika wamejiamulia hatma zao, kujipatia ukombozi wa taifa na uhuru wa nchi, na kujitahidi kujitafutia njia za kujiendeleza kwa kujitegemea. Baada ya kuingia karne mpya, uchumi wa Afrika umeonesha nguvu kubwa ya uhai, na umetimiza ongezeko la zaidi ya asilimia 5 kwa zaidi ya miaka 10 mfululizo, na kufanikiwa kuhimili msukosuko wa fedha wa kimataifa. Kwa ujumla, jamii ya Afrika imedumisha utulivu, uchumi wake umetimiza ongezeko la kasi, hali ambayo inaifanya Afrika ijitokeze duniani.

    Siku tatu zilizopita, nilipotoa hotuba kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika nilisema, Afrika imekuwa ncha moja ya dunia katika pande tatu. Kwanza, Afrika ina nchi 54 ambazo zinatoa sauti kwa kauli moja, na kuifanya Afrika kuwa ncha moja muhimu katika jukwaa la siasa la dunia, Pili, thamani ya jumla ya uchumi wa Afrika imezidi dola za kimarekani trilioni mbili. Mwaka 2013, nchi 7 kati ya 10 zenye ongezeko la kasi la uchumi duniani zilikuwa za bara la Afrika, hali ambayo imeifanya Afrika kuwa ncha moja muhimu katika ongezeko la uchumi wa dunia. Tatu, Afrika ina makabila zaidi ya 1500 na lugha zaidi ya 2000, ambazo zinaonesha ustaarabu na utamaduni wenye aina nyingi, na kuifanya Afrika iwe ncha yenye rangi mbalimbali katika ustaarabu wa binadamu. Katika miundo ya kiuchumi na kisiasa ya kimataifa, ni bora kuwa na ncha nyingi kuliko kuwa na ncha chache. Kujitokeza kwa Afrika na kuwa ncha mpya kumeifanya dunia iwe na demokrasia zaidi, iwe na utulivu zaidi, iwe na uhai zaidi, rangi nyingi zaidi, na pia kunasaidia kuhimiza amani na maendeleo ya dunia.

    Mabibi na mabwana,

    Kufaidika ongezeko la uchumi kwa haki na usawa kumekuwa wazo la kujiendeleza linalokubalika duniani. Kutimiza lengo la kuongeza ajira, na kupata maendeleo kwa haki na uwiano ndio kujipatia ongezeko katika hali ya kupata fursa kwa usawa, na kutimiza maendeleo yenye uwiano kati ya nchi na kanda pia ni kupata ongezeko la aina hiyo. Ushirikiano wa kunufaishana katika ya China na Afrika umeboresha maisha ya watu wapatao zaidi ya bilioni 2.4, na kuhimiza maendeleo lenye uwiano ya uchumi wa dunia, ushirikiano huo wenyewe ndio kujipatia ongezeko kubwa zaidi katika hali ya kupata fursa kwa usawa katika dunia.

    Afrika ni bara lenye nchi nyingi zinazoendelea, ingawa uchumi wa baadhi ya nchi za Afrika umeanza kupiga hatua kwa kasi, lakini bado unakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo miundo mbinu hafifu, ukosefu wa nafasi za ajira na idadi kubwa ya watu yenye matatizo ya kiuchumi. China ni nchi inayoendelea yenye idadi kubwa zaidi ya watu na ardhi kubwa zaidi duniani, ingawa thamani ya jumla ya uchumi wake iko kwenye nafasi za mbele duniani, lakini China ni nchi ya 100 hivi kwenye orodha ya Umoja wa Mataifa kuhusu kiwango cha maendeleo ya binadamu. China na Afrika zinakabiliwa na masuala yanayofanana, maendeleo ya kila upande yatatoa fursa kwa upande mwingine. Baada ya kuingia karne hii, uchumi wa China umeongezeka kwa kasi, na kuhimiza uuzaji nje wa bidhaa za Afrika, hali ambayo imeunga mkono ongezeko la uchumi wa Afrika; kwa upande mwingine, uchumi wa Afrika una mustakbali mkubwa, na umevutia kampuni nyingi za China kuwekeza barani Afrika, hali ambayo pia imepanua nyanja za maendeleo ya uchumi wa China. Afrika ina mahitaji katika ujenzi wa miundo mbinu na maendeleo ya viwanda, na China ina uwezo wa kutosha katika maeneo hayo. Uchumi wa pande hizo mbili uko katika hali ya kunufaishana, ushirikiano kati ya China na Afrika hakika utatoa nguvu kubwa ya msukumo kwa maendeleo ya pande hizo mbili.

    Mabibi na mabwana,

    "Mapiramidi na Ukuta Mkuu havikujengwa na mtu mmoja peke yake", kuwa na mshikamano na ushirikiano ndio kunaweza kupata maendeleo kwa pamoja. Katika miaka 50 iliyopita, waziri mkuu wa China marehemu Zhou Enlai alipofanya ziara barani Afrika, alieleza hatua tano zinazoiongoza China kwenye uhusiano kati yake na Afrika na kanuni nane za kutoa misaada kwa Afrika, China siku zote inashikilia kanuni hizo. Mwaka jana, rais Xi Jinping wa China alipotembelea Afrika, alitoa wazo la China kuhusu kuuendeleza uhusiano na Afrika kwa "udhati, uhalisi, udugu na uwazi", China itashikilia wazo hilo na kutumia vizuri fursa mpya za kihistoria katika kusukuma mbele kanuni nne na miradi mikubwa sita kuhusu ushirikiano kati yake na Afrika, yaani kushikilia kanuni nne za kutendeana kwa udhati na usawa, kuongeza mshikamano na hali ya kuamiana, kunufaika na ongezeko la uchumi kwa haki na usawa, kuvumbua njia ya kufanya ushirikiano katika mambo halisi, kutekeleza miradi mikubwa 6 kuhusu ushirikiano katika shughuli za viwanda, mambo ya fedha, kupunguza umasikini, uhifadhi wa mazingira, maingiliano ya kiutamaduni na kulinda amani na usalama, ambapo tungetumia vizuri jukwaa la Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, kujitahidi kufuata mahitaji mapya ya kujiendeleza kwa Afrika, ili kuinua kiwango cha ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuufanya uhusiano wa aina mpya wa wenzi wa kimkakati kati ya pande hizi mbili uendelezwe kwenye kiwango kipya.

    Kutimiza lengo la ongezeko la uchumi katika hali ya kupata fursa ya usawa, ni lazima kufanya kwanza ujenzi wa miundo mbinu hasa ya mawasiliano. Tutaendelea kuweka mkazo katika ujenzi wa miundo mbinu wakati wa kufanya ushirikiano na nchi za Afrika, kwenye msingi wa mipango ya utekelezaji tuliyopanga pamoja na Umoja wa Afrika kuhusu kufanya ujenzi wa miundo mbinu wa kuvuka mipaka ya nchi au eneo, ili kusukuma mbele ushirikiano na mawasiliano barani Afrika. Nilipojadilia na viongozi wa nchi za Afrika, niliona tunaweza kufanya ushirikiano katika mitandao mikubwa. Kwanza ni mtandao wa reli ya mwendo kasi barani Afrika. Eneo la jumla la Afrika linachukua asilimia 23 la maeneo ya nchi kavu ya dunia, lakini urefu wa jumla wa reli barani Afrika unachukua asilimia 7 tu ya ule wa dunia, tena nchi 13 za Afrika bado hazina reli. Siku chache zilizopita, mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Bibi Zuma alisema, Afrika ina "ndoto ya karne", yaani kujenga mtandao wa reli ya mwendo kasi ambao unaweza kuunganisha miji mkuu ya nchi zote za Afrika. Upande wa China unapenda kufanya juhudi za kuingia katika pendekezo hilo, na kushirikiana na nchi za Afrika katika kuanzisha mradi wa kujenga reli ya mwendo kasi, kufanya ushirikiano kwa pande zote katika kusanifu, kupanga mipango, kuandaa zana na vifaa na kufanya usimamizi, tena inapenda kuanzisha kituo cha utafiti na uendelezaji wa reli ya mwendo kasi barani Afrika, ili kusaidia ujenzi wa "mradi wa karne" wa reli hii ya Afrika, ambapo tunaweza kupiga hatua ya kwanza katika eneo dogo. Pili ni mtandao wa barabara za mwendo kasi barani Afrika. Hivi sasa kiwango cha barabara za kawaida na barabara za mwendo kasi barani Afrika kinachukua moja ya nne na moja ya 10 cha kile cha wastani cha dunia, hivyo Afrika ina nguvu kubwa ya kuendeleza ujenzi wa barabara. Viongozi wengi wa Afrika wameeleza matumaini yao ya kupanua ushirikiano na Afrika katika ujenzi wa barabara za mwendo kasi, na kujenga mtandao wa reli za mwendo kasi, upande wa China unaunga mkono na kupenda kuongeza ushirikiano na upande wa Afrika, ili kuzifanya barabara za Afrika ziunganishwe siku hadi siku na ziwe mtandao mkubwa. Tatu ni kujenga mtandao wa usafiri wa ndege kwenye eneo la Afrika. Hivi sasa mahitaji kwenye soko la usafiri wa ndege barani Afrika yanaongezeka kwa haraka, lakini bado kuna upungufu mkubwa wa viwanja vya ndege, njia za usafiri wa ndege hasa kwenye njia ya matawi ya usafiri wa ndege, huku China ina uwezo na uzoefu wa kujenga viwanja vya ndege na kufanya usimamizi husika, na ndege zilizosanifiwa na kutengenezwa na China pia zinaweza kutosheleza mahitaji kwenye soko la Afrika. Upande wa China unatetea kutekeleza "Mpango wa ushirikiano kati ya China na Afrika kuhusu usafiri wa ndege eneo kwa eneo", China inapenda kusukuma mbele maendeleo ya shughuli za usafiri wa ndege kwenye eneo la Afrika kwa kupitia kuanzisha makampuni ya ubia ya usafiri wa ndege, kutoa ndege za usafiri kwenye njia ya matawi ya usafiri wa kiraia, kusaidia kuwaandaa watu wenye ujuzi maalum wa usafiri wa ndege, na kujenga vifaa na zana za kuambatana na kuhakikisha usafiri wa ndege. Aidha, upande wa China unapenda kufanya ushirikiano na Afrika katika kuhimiza ujenzi wa miundo mbinu ya uzalishaji wa umeme, mawasiliano ya habari na posta. Tukitaka kujipatia maendeleo halisi, tunapaswa kufanya vizuri kwanza ujenzi wa miundo mbinu. Upande wa China unapenda kutoa msaada wa fedha, wataalamu na teknolojia kwa ajili ya ujenzi wa mtandao wa miundo mbinu ya Afrika.

    Hapa ningependa kusisitiza kwanza, ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika ni wa dhati na ulio wazi, teknolojia za kisasa na uzoefu wa usimamizi wa kufaa ilivyonavyo China vyote vitatolewa ili nchi za Afrika zinufaike pia; katika miradi yote ambayo upande wa China utakayoshiriki kwenye ujenzi na uendeshaji wake, tunaweza kuchukua njia za ubia au ushirikiano na upande wa China. Upande wa China pia unapenda kuongeza ushirikiano na mashirika ya kimataifa na nchi husika katika kujadili ushirikiano kati ya pande tatu au pande nyingi chini ya kanuni za "Afrika inakubali, Afrika inahitaji na Afrika inajishirikisha", ili kutoa mchango kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo na ujenzi wa Afrika .

    Kazi muhimu ya kujipatia ustawi kwa Afrika ni kuendeleza viwanda. Sisi tunaunga mkono kuvifanya viwanda vinavyofaa ambavyo vinatumia nguvu kazi nyingi vihamishe kwanza barani Afrika, kuyaunga mkono makampuni ya China yaendeleze shughuli zao barani Afrika kwa kupitia kuwaajiri wafanyakazi wengi zaidi wenyeji wa huko, kuongeza nafasi za ajira zisizo za kilimo katika nchi za Afrika, hasa ajira zile zinazowafaa vijana wa huko. Siku chache zilizopita, nilitembelea miradi ya uwekezaji ya makampuni ya China nchini Ethiopia, nilifahamishwa kuwa, wafanyakazi wenyeji wa huko wanachukua asilimia 90, serikali ya China inafurahia hali hiyo na inayataka makampuni ya China yafanye hivyo. Wakati huo huo, tunaunga mkono Afrika kuongeza uzalishaji wa nafaka, na kukuza viwanda vya utengenezaji wa mazao ya kilimo vyenye ufanisi. Upande wa China pia unapenda kuhimiza Afrika ibadilishe njia ya kuendeleza shughuli za maliasili za nishati, ipanue shughuli zake kuendelea kutunga mipango ya utafutaji, kufanya usambazaji na uendeshaji, kusafisha mafuta na kuzalisha umeme; kuongeza kazi ya kutengeneza maliasili barani Afrika, na kuifanya nguvu yake bora ya maliasili iwe nguvu bora ya kiuchumi, ili kuongeza kihalisi uwezo wa kujiendeleza.

    Kukidhi mahitaji ya dharura na kutoa msaada bila kukawia ni desturi wanazofuata wachina. Ingawa China bado ni nchi inayoendelea, lakini kwa kweli imekuwa kundi kuu moja la uchumi duniani, hivyo China itafanya kama ilivyofanya siku zote na kadiri iwezavyo katika kupanua ukubwa wa msaada wake kwa Afrika na kuinua sifa ya utoaji wa msaada huo. Tutatumia nusu ya msaada wa fedha tunazotoa kwa nchi za nje katika bara la Afrika, tutatilia mkazo zaidi utoaji msaada kwa ajili ya Afrika kuondoa umasikini, kazi ya kilimo, usafi, maji safi ya kunywa, kukinga na kupunguza maafa, ili kuwasaidia watu wa Afrika watatue matatizo mengi katika maisha ya kawaida. China itaendelea kutuma madaktari kwenye nchi za Afrika na kutekeleza mpango wa utoaji wa huduma za matibabu ili kuwasaidia wagonjwa wenye tatizo la mtoto wa jicho waweze kuona vizuri tena. Ningependa kusisitiza kuwa, misaada yote ya China itatolewa bila masharti yoyote ya kisiasa, kutoingilia kati mambo ya ndani, na kutotoa matakwa ya kuwafanya watu waone taabu ya kuyatimiza.

    Kuhifadhi mazingira wakati wa kujiendeleza, na kujiendeleza wakati wa kuhifadhi mazingira ni muhimu zaidi. Tutatilia mkazo zaidi ushirikiano kati ya China na Afrika katika kuendeleza shughuli bila kuchafua mazingira, kuyahimiza makampuni ya China yanayofanya shughuli zao barani Afrika yatekeleze majukumu yao ya kijamii, kuzuia kithabiti hali ya kuchimba madini kiharamu na kutoa uchafuzi kwa kuvunja sheria, kutoa adhabu kali kwa vitendo vya kuvunja sheria kama vile kufanya magendo ya mbao nyekundu na pembe za ndovu. Serikali ya China itatoa msaada wa dola za kimarekani milioni 10 kwa Afrika katika kulinda wanyamapori wa Afrika, kuhifadhi viumbe anuai, na kusukuma mbele maendeleo endelevu ya Afrika.

    Biashara na uchumi na utamaduni ni "magurudumu mawili yanayohimizana katika ushirikiano kati ya China na Afrika. Upande wa China utajiunga na upande wa Afrika katika kuhimiza biashara na uchumi, kuendelea kupanua ukubwa wa uwekezaji, kuimarisha maingiliano ya kiutamaduni kati ya watu wa China na Afrika, kuzidisha kwa kina ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, elimu, utamaduni, vyombo vya habari na michezo, kupanua mawasiliano kati ya wanawake na vijana, kuimarisha ushirikiano katika kulinda amani na usalama, kuhimiza mawasiliano kati ya mabunge, vyama, mashirika na jumuiya, washauri mabingwa na raia wa kawaida, ili tamaduni za kale za pande mbili zing'are zaidi kupitia maingiliano kati yao. Nina imani kuwa, tukitegemea urafiki wa China na Afrika, na kuufanya ushirikiano katika sekta za uchumi na biashara na utamaduni, tutaweza kusukuma ushirikiano kati ya China na Afrika uendelee kwa kasi, ili China na Afrika zipige hatua imara na madhubuti na kusonga mbele zaidi katika njia ya kujipatia maendeleo kwa pamoja.

    Mabibi na mabwana,

    Tukijadili ushirikiano kati ya China na Afrika, ningependa kueleza zaidi kuhusu uchumi wa China, hali yake ya sasa na mwelekeo wake. Katika zaidi ya miaka 30 iliyopita, uchumi wa China uliongezeka kwa kasi, hivi sasa China inashika nafasi ya pili duniani kwa ukubwa wa uchumi wake. Lakini China bado ni nchi kubwa inayoendelea, pato la taifa kwa wastani wa watu wa China ni dola za kimarekani elfu 6 tu, kiasi ambacho hakijafikia kile cha wastani duniani. Kuna pengo kubwa la maendeleo kati ya miji na vijiji nchini China, ambapo umaalum wa nchi inayoendelea unaonekena kwa udhahiri, kwa mfano wananchi wake zaidi ya milioni 700 ni wakulima wenye pato lisilozidi dola za kimarekani 1,400 kwa wastani, huku wachina wapatao zaidi ya milioni 200 bado wanaishi katika hali ya umaskini kwa mujibu wa vigezo vya benki ya dunia. Vilevile zaidi ya asilimia 60 ya wachina wanaishi katika sehemu za magharibi ya kati na kaskazini mashariki, ambapo pato la taifa kwa wastani wa watu hao halijafikia nusu ya wenzao wanaoishi katika sehemu za pwani. Ndiyo maana bado kuna safari ndefu sana kwa China kujenga mambo ya kisasa.

    Mwaka jana uchumi wa China uliongezeka kwa asilimia 7.7, na katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu ongezeko hilo lilikuwa asilimia 7.4, takwimu hizo zinaonesha hali nzuri ya ongezeko la kasi kiasi kutokana na ukubwa wa uchumi wa China ,na kwa kulinganisha hali yake katika siku za nyuma. Hata hivyo ongezeko hilo limepungua kidogo kutokana na sababu hali yake halisi. Hivi sasa ukubwa wa uchumi wa China umezidi dola za kimarekani trilioni 9, na ukiongezeka kwa asilimia 7.5 unaleta dola za kimarekani bilioni 700 hivi, kiasi ambacho kinalingana na uchumi wa nchi iliyoendelea ya ukubwa wa kati. Pia napenda kusema China bado ina msingi imara ya kudumisha ongezeko la uchumi katika siku za mbele, kwani pengo la kiuchumi kati ya miji na vijiji, linathibitisha kuwa bado kuna nguvu na nafasi kubwa kwa ukuaji wa uchumi wa China.

    Katika miaka mingi iliyopita, China ilikuwa inafanikisha ongezeko la uchumi la asilimia zaidi ya 10, hivi sasa tumelegeza kidogo kasi hiyo kwa sababu tunazingatia zaidi ubora na ufanisi wa ongezeko hilo, ili tufaidike na ongezeko la uchumi kwa haki na usawa na tuwe na maendeleo endelevu zaidi. Mageuzi ni injini ya maendeleo. Maendeleo ya kasi iliyopata China yalitokana na mageuzi, na maendeleo yake yenye ufanisi katika siku za baadaye pia yatatokana na mageuzi. Kubadilisha muundo wa uchumi kunaweza kuleta manufaa kwa hivi sasa na kwa siku za baadaye. Kwa hiyo uchumi wa China hakika utapata ongezeko kubwa zaidi kutokana na hatua mbalimbali za mageuzi, ambazo zinalenga kubadilisha muundo wa uchumi, kuboresha muundo wa shughuli za viwanda, kuendeleza miji yenye hali nzuri ya kimaisha na kufanikisha maendeleo ya pwani yaenee hadi sehemu za ndani. Katika mageuzi yetu, hatua za kuboresha maisha ya watu zina umuhimu mkubwa katika kuongeza matumizi na mahitaji ya soko la ndani. Tutazidi kufanya mageuzi ya mfumo wa kugawanya mali ili watu wengi zaidi waingie katika kundi la watu wenye pato la kati, pia tutaanzisha mfumo ulio salama wa huduma za jamii, kuongeza matumizi ya wananchi wapatao bilioni 1.3, na kuhimiza maendeleo ya jamii. Hayo yote hakika yatakuwa msukumo mkubwa zaidi utakaoleta ongezeko la uchumi wa China.

    Hivi sasa tunapojadili maendeleo ya China, mambo yanayotajwa ni pamoja na kuongeza nafasi za ajira, kuleta maendeleo yenye uwiano, kufanikisha haki na usawa, kuboresha maisha ya watu, kuhimiza maendeleo ya jamii, hiyi ndio tafsiri ya kufaidika ongezeko la uchumi katika hali ya kupata fursa ya usawa. Tuna imani na uwezo wa kutimiza asilimia 7.5 ya ongezeko la uchumi wa China, ambalo lengo hilo liliwekwa kwa mwaka huu na miaka ijayo katika kipindi kirefu, hali ambayo itanufaisha nchi mbalimbali za Afrika na uchumi wa dunia.

    Mabibi na mabwana,

    Mchakato wa maendeleo ya Nigeria na nchi nyingi barani Afrika, umeashiria mustakbali mzuri wa bara hilo. Nikiwa hapa na kutupia macho bara zima la Afrika, nimeona mto Nile, mlima Kilimanjaro na jangwa la Sahara, zaidi ya hayo nimevutiwa na bara lenye nguvu kubwa ya uhai na matumaini. Wachina wa zama za kale walisema, wenye nia moja ndio wanaofanikisha mambo. Sisi tunapenda kutendeana kwa usawa na watu wa Afrika, kufanya ushirikiano wa dhati na kusonga mbele bega kwa bega, ili kusukuma mbele maendeleo ya Afrika na kutoa mchango kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya dunia.

    Kwa kumaliza hotuba hii, nautakia mafanikio mema mkutano huu.

    Asanteni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako