• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China ayataka makampuni ya China yatoe kipaumbele mradi wa kuboresha maisha ya watu wa nchi wanayowekeza

    (GMT+08:00) 2014-05-09 10:36:16

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ameyataka makampuni ya China yatafuta kunufaishana wakati yanafanya biashara zao nje ya China. Bw. Li ameyasema hayo alipohuhudhuria mkutano kuhusu mradi wa kuboresha maisha ya watu katika nchi za nje mjini Luanda, Angola. Amesema ingawa makampuni ya China na ya nchi za nje yanashindana katika uchumi wa soko huria, makampuni hayo yanapaswa kufanya ushirikiano unaonufaisha pande mbili. Ameongeza kuwa makampuni ya China na Wachina waliopo nchi za nje wanatakiwa kufuata sheria za huko, kuheshimu mila na desturi, kutekeleza majukumu ya kijamii kadri iwezekanavyo, kulinda jina la China.

    Jana Bw Li pia aliwatembelea wafanyakazi wa China wanaotoa msaada wa matibabu nchini Angola, na. shule inayotoa mafunzo ya kazi iliyojengwa kwa ushirikiano wa China na Angola, na kushiriki kwenye sherehe ya kufunguliwa kwa shule hiyo akiambatana na makamu wa rais wa Angola Bw Manuel Domingos Vicente. Shule hiyo inatoa mafunzo ya kazi bure kwa vijana maskini wenye umri wa 16 hadi 25 ili kuwasaidia kupata ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako