• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China apendekeza kushirikiana na nchi za Afrika kujenga "mitandao mitatu ya miundo mbinu" katika bara hilo

    (GMT+08:00) 2014-05-09 10:42:40

    Waziri mkuu wa China apendekeza kushirikiana na nchi za Afrika kujenga "mitandao mitatu ya miundo mbinu" katika bara hilo

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema China inapenda kushirikiana na nchi za Afrika katika ujenzi wa mitandao ya reli ya mwendo kasi, barabara ya mwendo kasi na usafari wa ndege kwenye eneo la Afrika.

    Bw. Li ameyasema hayo alipotoa hotuba kwenye mkutano wa kilele wa Afrika wa Baraza la uchumi la dunia unaoendelea nchini Nigeria. Kwenye hotuba hiyo Bw Li alisema China inapenda kutoa msaada wa fedha, wataalamu na teknolojia kwa ajili ya ujenzi wa mtandao wa miundo mbinu ya Afrika.

    Bw. Li pia amesema, China inaunga mkono kuvifanya viwanda vinavyofaa ambavyo vinatumia nguvu kazi nyingi vihamishwe kwanza barani Afrika, na kuunga mkono Afrika kuongeza uzalishaji wa nafaka, na kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta zisizochafua mazingira. Amesisitiza kuwa, China inatoa misaada bila ya masharti yoyote ya kisiasa, kutoingilia kati mambo ya ndani, na haitoi matakwa ya kuwafanya watu waone taabu ya kuyatimiza.

    Mwenyekiti wa Baraza la uchumi la dunia Bw. Klaus Schwab na rais Goodluck Jonathan wa Nigeria pia walitoa hotuba na kusifu sera za China kwa Afrika na ushirikiano kati ya Afrika na China. wamesema baraza hilo na nchi za Afrika zinapenda kuimarisha ushirikiano na China, ili kusukuma mbele maendeleo endelevu ya Afrika na dunia nzima.




    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako