• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hotuba iliyotolewa na waziri mkuu wa China kwenye Baraza la uchumi la dunia yavutia mwitikio mkubwa

    (GMT+08:00) 2014-05-09 16:51:55

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ambaye alikuwa ziarani nchini Nigeria jana alitoa hotuba kwenye mkutano wa 24 wa kilele wa Afrika wa Baraza la uchumi la dunia unaofanyika mjini Abuja, akisisitiza kuwa kujitokeza kwa Afrika kunasaidia amani na maendeleo ya dunia, na ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika na unahimiza maendeleo yenye uwiano ya uchumi wa dunia wenye ongezeko kubwa linalonufaisha watu kwa haki na usawa. Hotuba yake imevutia mwitikio mkubwa.

    Bw. Li Keqiang amesema, uchumi na utamaduni ni magurudumu mawili ya ushirikiano kati ya China na Afrika, China itashirikiana na Afrika kuimarisha mawasiliano katika kila sekta ili kuzifanya pande hizo mbili zenye ustaarabu wa kale zinufaishane kwa njia ya kufundishana, na kuhimiza ushirikiano huo uendelee kupiga hatua.

    Hotuba ya Bw. Li Keqiang ilipigiwa makofi mara nyingi, na hatua na mitizamo aliyotoa kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika imezua mjadala mkubwa kwenye mkutano huo. Mjumbe maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika Bw. Zhong Jianhua anasema:

    "Hotuba yake imevutia mwitikio mkubwa kwenye mkutano huo, nchi za Afrika zimetoa maoni ya kukubaliana. Papo hapo kwenye mkutano huo kulikuwa na marais na mawaziri wakuu wa nchi za Afrika walisema kwamba wamesikia wazi udhati wa China katika kutoa misaada kwa Afrika."

    Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Benki ya Standard Chartered barani Afrika Bibi Diana Layfield alisema hotuba ya waziri mkuu Li Keqiang imemuonesha kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika unaleta fursa kwa Afrika.

    "Waziri mkuu Li Keqiang ameonesha kwa mtizamo wa kina mustakbali wa ushirikiano kati ya China na Afrika, na kufungua ukurasa mpya kwa uhusiano kati ya China na Afrika, naona itakuwa ni fursa ya kusisimua kwa Afrika."

    Naye Bw. David Church kutoka kampuni ya ushauri wa kisheria ya kimataifa ya Uingereza alisema amevutiwa sana na mtizamo wa Bw. Li Keqiang unaoshikilia usawa na kunufaishana katika ushirikiano kati ya China na Afrika.

    "kinachonivutia zaidi ni jinsi China inavyoisaidia Afrika, China hailengi kupata maslahi tu kutoka kwa Afrika, Bw. Li Keqiang ameweka bayana mtizamo wa China wa kuisaidia Afrika kwa udhati na uhalisi, ambao kweli unastahili kusifiwa."

    (Simba, Fadhili)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako