• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji na Angola

    (GMT+08:00) 2014-05-09 18:37:51

    Waziri wa biashara wa China Bw. Gao Hucheng ambaye anafuatana na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang katika ziara yake nchini Angola amesema, China itapanua ushirikiano wa uwekezaji kati yake na Angola.

    Bw. Gao Hucheng amesema hayo alipohojiwa na waandishi wa habari mjini Luanda. Amesema ili kuisaidia Angola kuongeza uzalishaji wa nafaka, China inapenda kuanzisha mapema kituo cha vielelezo vya kilimo, na upandaji wa mbegu bora, huku ikiendelea na miradi ya sasa ya mafunzo ya kilimo na ujenzi wa miundo mbinu.

    Pia amesema, serikali ya China itaendelea kuunga mkono makampuni ya China kushiriki kwenye miradi ya ujenzi wa miundo mbinu ya reli, barabara, na mtandao wa umeme, pamoja na kuhamisha teknolojia, kuandaa wataalamu wenyeji, na kuongeza nafasi za ajira nchini humo, ili kuisaidia Angola kutimiza maendeleo endelevu.

    (Upendo, Carol, Simba)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako