• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China azungumza na rais wa Angola

    (GMT+08:00) 2014-05-10 09:46:51

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang amesema China inapenda kuendelea kushirikiana na Angola katika masuala mbalimbali, kuimarisha mawasiliano kati ya vyama na kubadilishana maoni kuhusu uongozi wa nchi, kuongeza uratibu katika masuala ya kimataifa na ya kikanda ili kuendeleza zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Bw. Li Keqiang amesema hayo alipozungumza na rais Jose Eduardo dos Santos wa Angola mjini Luanda. Bw. Li amesema China inatilia maanani uhusiano na Angola, na kuichukulia Angola kuwa rafiki muhimu wa ushirikiano, na inaunga mkono mkakati wa "maendeleo, utulivu na ajira" inaofuata Angola katika kuongoza nchi.

    Rais dos Santos amesema China ni nguvu muhimu katika kulinda amani na maendeleo ya bara la Afrika na dunia nzima, pia ni rafiki na mwenzi anayetegemewa wa Angola, na kuimarisha ushirikiano kati ya Angola na China kuna umuhimu mkubwa kwa maendeleo endelevu ya Angola, na Angola inapenda kupanua ushirikiano wa kunufaishana na China, na kukaribisha makampuni ya China kuongeza uwekezaji na kushiriki kwenye ujenzi wa uchumi na jamii nchini Angola. Baada ya mazungumzo hayo viongozi hao wawili walishuhudia kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano katika sekta za uchumi, teknolojia, matibabu, fedha na mawasiliano kati ya watu.

    Habari nyingine zinasema waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na rais dos Santos wa Angola walikutana kwa pamoja na waandishi wa habari baada ya mazungumzo kati yao.Bw. Li amesema wamekubaliana kuunda kikundi cha kikazi kupanga maeneo yatakayofanyiwa ushirikiano kati ya China na Angola, na China itaisaidia Angola katika ujenzi wa miundo mbinu, kuimarisha ushirikiano katika mambo ya kilimo na kubadilisha uzoefu wa ufundi, kuongeza mawasiliano kati ya watu na China itatoa mafunzo ya rasilimali ya watu kwa Angola ili kupanua wigo wa ajira kwa vijana wa Angola.

    Naye rais dos Santos amesema ziara ya Bw. Li Keqiang nchini Angola itasukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako