• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri aahidi China kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na Kenya

    (GMT+08:00) 2014-05-10 15:38:08

    Waziri wa Biashara wa China Bw Gao Hucheng amesema China iko tayari kufanya juhudi na Kenya ili kupanua ushirikiano katika sekta ya uwekezaji, miundo mbinu, usafiri wa ndege wa kikanda, maisha ya watu na uhifadhi wa mazingira.

    Waziri huyo amesema China imekuwa mwenzi mkubwa wa pili wa kibiashara wa Kenya, na maua, chai na ubani vinaagizwa kwa wingi na China kutoka Kenya.

    Habari zinasema mwaka jana thamani ya biashara kati ya China na Kenya ilifikia dola za kimarekani bilioni 3.27, kiasi ambacho ni kikubwa zaidi katika historia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako