• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China aanza ziara nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2014-05-10 15:59:48

    Kutokana na mwaliko wa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amewasili mjini Nairobi, na kuanza ziara yake rasmi nchini Kenya.

    Bw. Li amesema anatarajia kubadilishana maoni kwa kina na viongozi wa Kenya kuhusu masuala yanayozihusu nchi zao na mausala yanayofuatiliwa na pande hizo mbili, ili kuufanya uhusiano wa kiwenzi wa kuaminiana na ushirikiano wa kunufaishana upate maendeleo zaidi.

    Katika ziara hiyo, Bw. Li atakutana na viongozi wa serikali ya Kenya, watu kutoka sekta mbalimbali, pamoja na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Bw. Achim Steiner, na mkurugenzi mtendaji wa Shrika la Makazi la umoja huo (UN-HABITAT)Bw. Joan Clos.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako