• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuwekeza katika sekta ya usafiri wa anga nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2014-05-10 20:38:45

    Shirika la ndege la Hainan la China linatarajiwa kusaini makubaliano na shirika la ndege za mizigo la Kenya Astral ili kutumia kwa pamoja soko la nchi za Afrika Mashariki.

    Makubaliano hayo yatasainiwa katika kipindi hiki cha ziara ya waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang nchini Kenya ambayo ilianza jana na kumalizika kesho.

    Makubaliano hayo pia yatahusisha mfuko wa maendeleo kati ya China na Afrika, ulioanzishwa na China mwaka 2007 ili kusaidia uwekezaji wa China barani Afrika.

    Kutokana na makubaliano hayo, shirika la ndege la Hainan litakuwa na hisa katika shirika la Astral na chombo hiki kipya cha ubia kitatoa huduma za usafiri wa ndege katika nchi za Afrika Mashariki huku Nairobi ikiwa ndio kituo chake kikuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako