• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na China zitaendelea kuimarisha ushirikiano kati yao na kutimiza maendeleo ya pamoja.

    (GMT+08:00) 2014-05-10 21:31:41

    Kenya na China zimesema zitaendelea kuimarisha ushirikiano kati yao na kutimiza maendeleo ya pamoja.

    Hayo yamekubaliwa kwenye mkutano kati ya rais Uhuru Kenyatta na Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ambaye anaendelea na ziara yake nchini Kenya.

    Bw. Li amesema China inapenda kuongeza kuagiza bidhaa nyingi zaidi kutoka Kenya, kuhamasisha kampuni za China kuwekeza nchini Kenya, kushirikiana na Kenya katika ujenzi na uendeshaji wa reli, bandari na kituo cha umeme kwa kutumia uzoefu na teknolojia iliyo nayo China, na kuimarisha ushirikiano katika kilimo na hifadhi ya mazingira na wanyama pori.

    Kwa upande wake, rais Kenyatta amesema Kenya inapenda kuongeza mawasiliano na kuimarisha ushirikiano na China katika nyanja mbalimbali ili kutimiza maendeleo ya pamoja. Ameongeza kuwa Kenya inapenda kuwa mlango wa kuingiza makampuni ya China barani Afrika.

    Baada ya mazungumzo hayo, viongozi hao wawili wameshuhudia kwa pamoja kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika uchumi, teknolojia, hifadhi ya wanyamapori, afya, kilimo, ufugaji na uvuvi na mambo ya fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako