• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Li Keqiang na rais wa Kenyatta wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2014-05-11 09:07:21
    Serikali ya Kenya imetia sahihi mikataba 17 ya kibiashara na China katika siku ya pili ya ziara ya waziri mkuu wa China Li Keiqiang. Mikataba hiyo ya biashara bali mbali inalengwa kuimarisha uchumi wa Kenya na ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili. China pia imetangaza kutumia shilingi milioni 860 katika kuhifadhi wanyama pori katika nchi tofauti barani Afrika. Ahmed Bahajj kutoka Nairobi anaripoti Siku ya pili ya ziara ya waziri mkuu wa China nchini Kenya Li Keiqiang ilishuhudia shughuli tofauti nchini. Katika hotuba yake kwa waandishi wa habari waziri Li keqiang ameahidi kuwa ushirikiano wa Kenya na China utazidi kuimarika. Li amesisitiza kuwa China itasaidia kuimarisha sekta ya viwanda ili kuimarisha ukuwaji wa uchumi nchini. Pamoja na hayo Waziri Li alitia sahihi mikataba 17 ya kibiashara baina ya China na Kenya. Mikataba hiyo ilitiwa sahihi na waziri wa biashara wa China Gao Huchen na waziri wa fedha wa Kenya Henry Rotich kwa niaba ya nchi hizi mbili. Katika hotuba yake fupi waziri Li alisema "Urafiki wetu na Kenya utadumu milele…Kenya ndio kituo chetu cha mwisho katika ziara hii.kwa wachina tunaamini kuwa cha mwisho kinadumu." Rais Uhuru Kenyatta amepongeza ushirikiano na usaidizi wa China katika miradi tofauti hususan sekta ya miundo msingi. "Ukiangalia maendeleo tulioyopta katika miundo msingi nchini katika miaka 10 ya ushirikiano wetu na China tumepata manufaa makubwa. Tunataka kuendelea na miradi hii .kama alivosema waziri uimarishaji wa miundo msingi utapunguza gharama ya kufanya biashara na pia kufungua nafasi za ajira miongoni mwa wanachi." Rais Uhuru Kenyatta aidha ameitaka China kupanua ushirikiano wake katika sekta ya utalii alipokutembelea mbuga ya kitaifa ya wanyama Nairobi. "Ni muhimu sana ushirikiano wa nchi hizi mbili uzingatie sekta ya turathi za kitaifa kama mbuga za kuhidafhi wanyama. Tuntaoa wito kwa wachina kuja hapa nchini katika ziara za utalii.tunawakaribisha waje kwa wengi watembee katika nchi yetu na kujionea mbuga za wanyama. Tunatumai kupokea idadi kubwa ya watlii kutoka China baada ya ziara ya waziri mkuu" Mbali na sekta ya biashara China pia imeahidi kutumia shilingi milioni 860 katika kuhifadhi wanyama pori katika nchi tofauti barani Afrika. Waziri Li Keiqiang ametangaza kuwa fedha hizo kutoka China zitatumika kufadhili harakati za kuboresha mazingira ya wanyama pori barani Afrika. Hatua hii inajiri ili kukabiliana na visa vya uwindaji haramu uliojitokeza kukithiri katika siku za hivi karibuni. Hii leo siku ya jumapili Waziri Li Keiqiang anatarajiwa kukutana na viongozi wengine wan chi za afrika mashariki akiwemo Rais Yoweri Museveni (Uganda), Jakaya Kikwete (Tanzania),Paul Kagame, Rwanda and Salva Kiir (South Sudan) kwa mazungumzo ya amani ,usalama na miundo msingi. Kabla ya kikao na viongozi hao Waziri Li pia anatarajiwa kutia sahihi rasmi mkataba wa ujenzi wa reli mpya ya kutoka Kenya Uganda hadi Rwanda. Viongozi hao wawili hawakubainisha rasmi kima cha fedha zitakazotumiwa katika miradi yote lakini ni thamani ya mabilioni ya pesa. Miongoni mwa miradi ilitiwa sahihi ni ya sejka ya elimu,kilimo,biashara na fedha. Baraza rasmi la ushauri litaundwa ili kufuatilia utekelezaji halali wa miradi iliyotiwa sahihi. Kenya inalenga kutumia ziara hii kuzidisha mapato ya kiniashara China nayo imeapa kutumia nafasi hii kupanua soko la bidhaa za Kenya. Waziri LiKeiqiang anatarajiwa kuwa nchi kwa siku tatu
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako