• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na naibu rais wa Kenya

    (GMT+08:00) 2014-05-12 10:22:29

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana asubuhi alikutana na naibu rais wa Kenya Bw. William Ruto.

    Bw. Li Keqiang amesema, Kenya ni kituo cha mwisho cha ziara yake barani Afrika, na amezungumza na rais Uhuru Kenyatta na kufikia makubaliano kuhusu mambo mengi na kushuhudia kusainiwa kwa nyaraka mbalimbali za ushirikiano. Bw. Li Keqiang pia ameishukuru Kenya kwa mapokezi mazuri, hali inayoonesha urafiki wa jadi, na Kenya inavyozingatia uhusiano kati yake na China. Bw. Li ameongza kuwa, China itaendelea kuiunga mkono Kenya katika kulinda utulivu, kuhimiza maendeleo ya uchumi, na kuboresha maisha ya wananchi.

    Bw. Ruto amesema, ziara ya waziri mkuu Li Keqiang imepata mafanikio makubwa, yatakayohimiza ushirikiano kati ya Kenya na China, na kati ya Afrika na China, na kuwaletea manufaa Wakenya na Waafrika kwa ujumla. Amesema Kenya inapenda kuimarisha ushirikiano na China hususan katika sekta za miundo mbinu, kilimo, utalii na mambo ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako