• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asisitiza kuimarisha ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2014-05-12 10:36:40

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alitembelea tawi la kituo cha televisheni cha taifa la China CCTV nchini Kenya, na kuangalia hali ya utendaji wa tawi hilo la CCTV, na uwezo wa kituo hicho kurusha matangazo. Bw. Li Keqiang amesema tawi hilo linapaswa kutangaza Afrika kwa mtazamo wa Waafrika. Amesema China na Afrika zinapaswa kuimarisha ushirikiano katika sekta ya vyombo vya habari, na kutangaza kwa hali halisi hali ya nchi zinazoendelea, ili nchi hizo zikiwemo nchi za Afrika zitoe sauti zao kwa dunia.

    Bw. Li Keqiang jana pia alitembelea kituo cha huduma kwa vijana cha Taifa la Kenya, ambacho ni idara ya kwanza yenye lengo la kuhamasisha watu kujenga makazi yao na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana baada ya Kenya kujipatia uhuru.

    (adela fadhili hasani)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako