• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Oviedo kulikosa kombe la dunia

    (GMT+08:00) 2014-05-12 16:09:03

    Mlinzi wa Everton Brayan Oviedo atashindwa kuikabili Uingereza kwenye michuano ya kombe la Dunia safari hii baada ya kuthibitika kuwa hadi michuano inaanza atakuwa bado hajapona. Oviedo ambaye ni Mcostarica amevunjika mguu wakati alipokuwa akicheza mechi ya kombe la FA huko Stevenage mwezi Januari, na kuamuriwa haraka kupumzika ili aendelee kujiuguza kwa muda uliobaki wa msimu. Mchezaji huyo alikuwa anaendelea vizuri na kudhaniwa atakuwa tayari kucheza wakati wa michuano ya kombe la dunia huko Brazil. Hata hivyo daktari wa timu ya Costa Rica Alejandro Ramirez amethibitisha kuwa anahitaji muda zaidi wa kupona na hatakuwa tayari kucheza mechi dhidi ya Uruguay tarehe 14 Juni au hata timu nyingine zilizopo kwenye kundi lake la D, ambazo ni Italy na Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako