• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cole ajiuzulu kuichezea Uingereza baada ya kutochaguliwa kwenye kikosi cha kombe la dunia

    (GMT+08:00) 2014-05-12 16:09:26

    Mchezaji wa Chelsea Ashley Cole hatocheza tena mechi za kimataifa kufuatia uamuzi wake wa kujiuzulu kwenye timu yake ya taifa ya Uingereza baada ya kuachwa kwenye kikosi kitakachocheza kombe la dunia. Mchezaji huyo mwenye miaka 33 amecheza kombe la dunia mara tatu. Winga wa kushoto wa Southampton Luke Shaw ambaye ana miaka 18, amejumuishwa ndani ya kikosi hicho baada ya kocha wa Uingereza Roy Hodgson kutangaza kikosi chake cha wachezaji 23 pamoja na wale wa stendbai. Cole amesema amepigiwa simu na Roy na kukubaliana kuwa Uingereza inahitaji wachezaji wachanga, hivyo ameahidi kwamba atakiunga mkono kikosi hicho kama mashabiki wengine. Roy amesema kutomchagua Cole kwenye kikosi hicho ni uamuzi mgumu alioufanya kwani amekuwa mshindani mkubwa kwa Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako