• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Blatter kugombania tena kwenye uchaguzi wa rais wa FIFA mwakani

    (GMT+08:00) 2014-05-12 16:10:29

    Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa FIFA Sepp Blatter ametangaza kuwa atagombea tena nafasi yake kwenye uchaguzi ujao mwakani. Mswisi huyo ambaye amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 1998, amethibitisha kuwa ataingia kwenye mbio za uchaguzi kwa kipindi cha tano. Akizungumza na gazeti la Uswisi Blick, Blatter mwenye miaka 77 amesema yeye sasa ni mgombea, ingawa mamlaka yake yameisha lakini kazi zake bado hazijaisha. Uchaguzi wa rais wa shirikisho hilo utafanyika Juni mwakani huko Zurich Uswisi. Mapema mwezi Oktoba Blatter alisita kuthibitisha nia yake hiyo lakini alidokeza kuwa angependa kuendelea na kazi yake ya sasa. Mwaka 2011 Blatter alishinda urais wa FIFA bila ya kikwazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako