• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Kenya zafikia makubaliano ya kufadhili kwa pamoja mradi wa ujenzi wa reli

    (GMT+08:00) 2014-05-12 17:07:16

    Serikali za China na Kenya zimesaini makubaliano mapya ya ujenzi wa reli itakayounganisha miji ya Nairobi na Mombasa. Makubaliano hayo yamesainiwa wakati wa ziara ya siku tatu ya waziri mkuu wa China Li Keqiang nchini Kenya.

    "Tunayakaribisha makampuni ya Kenya kutangaza bidhaa zao katika maonesho makubwa ya biashara ya China, serikali ya China itayapa ushirikiano mkubwa. Pia tutayashawishi makampuni mengi ya China kuwekeza nchini Kenya katika sekta ya viwanda, kuongeza uwezo wa uzalishaji hapa Kenya. Tunapenda kusaidia na kushiriki katika ujenzi wa maeneo ya viwanda hapa Kenya, kufanya ushirikiano wa pande mbili katika suala hili, ambalo tunatumai kuwa litainua nguvu ya ushindani ya Kenya"

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema serikali yake itajitahidi kuimrisha uhusiano kati yake na China

    "Hakuna shaka kuwa ushirikiano uliopo kati ya Kenya na China hususan katika miaka 10 hadi 12 iliyopita ni ushirikiano ambao umekuwa wa kuzinufaisha pande mbili, na umekuwa ni muhimu katika kutusaidia kufikia ajenda zetu za kijamii na kiuchumi. Tuna matarajio makubwa ya kuinua uhusiano huu, lakini pia kuangalia jinsi ya kupanua uhusiano huu, kama waziri mkuu alivyosema"

    Viongozi hao pia wamesaini makubaliano kadhaa yanayohusiana na mambo ya uchumi, fedha, na kilimo. Serikali ya China pia imetoa dola za kimarekani milioni 10 kusaidia ulinzi wa wanyamapori nchini Kenya.

    Kenya ni kituo cha mwisho cha ziara ya waziri mkuu wa China Li Keqiang katika nchi nne za Afrika.

    Mbali na makubaliano hayo, makubaliano mengine yaliyosainiwa wakati wa ziara yake Bw. Li Keqiang barani Afrika ni ya mradi wa ujenzi wa reli nchini Nigeria wenye thamani ya dola bilioni 13.1 za kimarekani. Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa masuala ya Afrika na Asia magharibi kwenye taasisi ya sayansi ya kijamii Bibi He Wenping alipozungumzia miradi hiyo ya miundo mbinu anasema:

    "Miundo mbinu ni eneo lenye nafasi kubwa zaidi ya maendeleo. Katika hotuba aliyotoa Bw. Li Keqiang kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika, alitaja miradi sita kati ya China na Afrika, moja kati ya miradi hiyo ni kuisaidia Afrika kuendeleza reli ya kasi, pamoja na barabara na usafiri wa ndege. Bw. Li amesema itakapofika mwaka 2020, biashara kati ya China na Afrika itakuwa mara mbili ya sasa, na uwekezaji barani Afrika kutoka China utazidi dola bilioni 100 za kimarekani, miundo mbinu ni moja kati ya maeneo yatakayosisitizwa sana. Aidha, kuboreshwa kwa miundo mbinu barani Afrika, kutakuwa msukumo mkubwa kwa uchumi wa bara hilo, na itahimiza ushirikiano kati ya nchi za Afrika."

    Kwa mujibu wa ripoti kuhusu ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika kwa mwaka 2013, mitaji mingi zaidi ya China barani Afrika inakwenda kwenye sekta ya huduma, na kuzidi ile iliyowekezwa kwenye sekta ya maliasili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako