• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atoa barua ya pongezi kwa mkutano wa tatu wa Baraza la watu wa China na Afrika

    (GMT+08:00) 2014-05-13 09:22:43

    Rais Xi Jinping amesema, ikiwa ni sehemu muhimu ya utaratibu wa mawasiliano na ushirikiano kati ya watu wa China na Afrika, baraza la watu wa China na Afrika limefanya kazi kubwa katika kuimarisha urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili na kusukuma mbele amani ya dunia.

    Rais Xi amesema ajenda kuu ya mkutano huo wa baraza hilo ya "watu wa pande mbili kushirikiana kupunguza umaskini", inafuatiliwa na watu wa pande zote mbili. Pia amesema baraza hilo kwa uhakika litaimarisha urafiki kati ya pande mbili na kuhimiza Afrika kutimiza malengo ya maendeleo ya Milenia.

    Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika ni msingi wa sera ya kidiplomasia ya China, na anaamini kuwa Baraza la tatu kati ya watu wa China na Afrika litaendelea kutia uhai kwenye uhusiano kati ya China na Afrika.

    Wakati huo huo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon ametoa pongezi kupitia video kwenye ufunguzi wa mkutano wa baraza hilo akisema anaunga mkono China na Afrika kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali. Amesema, China ni mwenzi mkubwa wa Afrika wa kibiashara na kimaendeleo, anatarajia kuwa pande hizo mbili zitaimarisha ushirikiano zaidi katika "kupunguza umaskini barani Afrika, kupambana na magonjwa na mabadiliko ya hali ya hewa, kuimarisha usimamizi ili matumizi ya raslimali barani Afrika yagawanywe kwa haki".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako