• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Iran alikosoa shirikisho la soka la Iran na wadhamini kwa kutoa vifaa visivyofaa

    (GMT+08:00) 2014-05-15 09:48:52

    Kocha wa timu ya taifa ya Iran katika michuano ya Kombe la dunia Carlos Queiroz na wachezaji wake wamelikasirikia shirikisho la mpira wa soka la Iran na wadhamini wao kwa kutoa soksi zinazosinyaa na viatu vidogo na ambavyo havitoshi kwa timu. Kutoelawana huko kumezidi kati ya kocha na shirikisho hilo kutokana na maandalizi finyu ya kombe la dunia la Brazil ambapo michuano inaanza Juni 12. Kocha huyo mreno alikuwa kwenye kambi ya mazoezi huko Afrika mwezi uliopita akiwa na wachezaji 12 tu. Ikiwa siku ndio zinazidi kukaribia kwa mechi yake ya kwanza ya kundi F dhidi ya Nigeria, Queiroz amekosoa wadhamini wao akisema vifaa walivyotoa havifai, na hali hiyo inaweza kuifanya Iran itolewe kwenye michuano hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako