• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya waziri mkuu wa China nchini Kenya yaongeza urafiki na ushirikiano

    (GMT+08:00) 2014-05-15 10:28:00

    Baada ya waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang kumaliza ziara kwa mafanikio nchini Kenya, ziara yake imetajwa kuwa imeongeza urafiki na uaminifu wa kimkakati kati ya China na Kenya. Balozi wa China nchini Kenya Liu Xianfa amesema Kenya ikiwa ni kituo cha mwisho katika ziara ya Li ya nchi nne za Afrika, imebeba jukumu la kuhimiza uhusiano kati ya China na Kenya. Amesema serikali ya Kenya imeipongeza ziara ya Bw. Li na kumkaribisha kwa itifaki ya ngazi ya juu. Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake Bw. William Ruto waliambatana na Li kwenye shughuli mbalimbali, na kuwaongoza mawaziri na maofisa waandamizi wa jeshi kukutana na kumuaga kwenye uwanja wa ndege. Rais Kenyatta alimwaandalia dhifa ya taifa Ikulu kwa ajili ya kumkaribisha Li, na pia alitoa makala kwenye vyombo vya habari vya Kenya kusifu uhusiano kati ya Kenya na China. Kwenye ziara ya Waziri Mkuu Li nchini Kenya, pande mbili zilisaini nyaraka 17 za ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako