Mlinda mlango wa Ufaransa Steve Mandanda amethibitisha kwamba hatashiriki michuano ya kombe la dunia nchini Brazil baada ya kupata majeraha ya shingo katika mechi iliyocheza Marseille ya ligi ya 1 ya Ufaransa. Mandanda mwenye miaka 27 alivaana na mshambuliaji wa Guingamp Mustapha Yatabare katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo iliyochezwa Jumamosi katika uwanja wa Velodrome ambapo Marseille iliibuka na ushindi wa 1-0. kupitia twiter Mandanda alithibitisha kutoshiriki kwenye kombe la dunia. Mandanda alitajwa pamoja na kipa Hugo Lloris wa Tottenham Hotspur na Mickael Landreau wa timu ya Bastia katika kikosi cha wachezaji 23 kwenye fainali za Brazil, ambapo kwa sasa Stephane Ruffie wa timu ya Saint-Etienne ambaye yupo katika majina ya wachezaji wa akiba anatarajiwa kuitwa ili kujiunga na kikosi hicho.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |