Jina la mpira rasmi utakaotumika katika mchuano wa kombe la dunia Brazil hapo Juni 12 ni Brazuca. Watengenezaji wa mpira huo Adidas pamoja na baadhi ya wachezaji wameusifu kwa shabaha na wepesi. Hata hivyo gwiji wa soka nchini Brazili Pele amewahimiza raia wenzake warekebishe mambo kutokana na kuonekana kuwa Brazil bado kuna hali ya wasiwasi. Balozi huyo wa soka mwenye umri wa miaka 73 Ametiwa wasiwasi na maandamano ya mara kwa mara ya kupinga matumizi ya pesa nyingi za kuandaa kombe la dunia. Maandamano hayo yameshangaza wengi kwani Brazil inahusudu na kusifika kwa ubingwa wao wa kusakata kandanda. Katika mkutano na waandishi habari huko Mexico Pele amenukuliwa akisema, ana taarifa kuwa tayari 25% ya mashabikii wa kigeni wameshavunja safari zao za kwenda Brazil kwa sababu ya maandamano hayo na kama yakiendelea basi wengine wengi huenda wakakata safari hizo na hivyo kuleta hasara kwa Brazil ya kukosa biashara hasa za kitalii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |