Nahodha na mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles Nwanko Kanu amesema anauhakika kwamba nchi yake safari hii itafanya vizuri zaidi na kuvuka hatua ya makundi katika michuano ya kombe la dunia nchini Brazil. Nigeria ipo kwenye kundi F pamoja na Argentina, Bosnia-Herzegovina na Iran. Kanu amesema ana uhakika kwamba mabingwa hao wa Afrika wataishinda Iran na Bosnia katika mechi zake mbili za awali na baadaye itavaana na Waamerika Kusini bila ya kikwazo kabla ya kuingia hatua ya mtoano. Kanu anatarajia mambo mazuri kutoka kwa Super Eagles na kuona kwamba itasonga mbele zaidi katika michuano hiyo kama ikishinda mechi mbili za mwanzo. Nigeria itapambana Iran Juni 16 na baada ya siku 5 itakwaana na Bosnia kabla ya kucheza na Argentina katika uwanja wa Porto Alegre Juni 25.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |