• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakala wa Yaya Toure akanusha kuhatarisha mkataba wa Yaya katika Manchester City

    (GMT+08:00) 2014-05-22 10:30:47

    Wakala wa Yaya Toure, Dimitri Seluk amekanusha madai kwamba maoni yake ya hivi karibuni kuhusu kiungo wa kati wa Manchester City yamehatarisha mkataba wa Yaya. Juzi Jumanne Seluk alisema Toure anaweza kuondoka City kwasababu klabu haikumpa heshima yake Toure katika siku yake kuzaliwa. Toure ambaye alijiunga na City mwaka 2010 akitokea Barcelona, alihusishwa kurejea tena klabu hiyo wakati Seluk alipotoa maoni hayo Jumanne. Alisema mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ivory Coast alidai kuwa amedharauliwa na mmiliki wa klabu wakati City ilipowasili United Emirate kusherehekea ushindi wa klabu bingwa ya Uingereza, hivyo kukasirishwa na kitendo hicho. Kiungo huyo alisema anaweza kuchezea klabu nyingine katika msimu ujao na kuongeza kuwa atajua hatma yake baada ya michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako