• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpira wa adidas utakaochezewa mechi ya fainali kwenye kombe la dunia "Brazuca final Rio" wazinduliwa

    (GMT+08:00) 2014-05-30 10:34:09

    Adidas imezindua rasmi mpira wa Brazuca final Rio utakaotumika kuchezewa mechi ya fainali kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Brazil. Mpira huo utakuwa ni sehemu muhimu katika pambano la tarehe 13 Julai wakati timu mbili zitakazofikia hatua ya fainali zitakapochuana. Brazuca Final Rio una rangi za kijani na dhahabu ambazo zinatokana na rangi za kikombe cha kombe la dunia na ni tofauti na mpira uliozinduliwa mwezi Disemba mwaka jana, ambao pia unaitwa Brazuca utakaochezewa mechi za kombe la dunia. Kabla ya uzinduzi wa Brazuca na Brazuca Final Rio, mipira hiyo ilifanyiwa majaribio kwa muda wa miaka miwili na nusu, na kuhusisha wachezaji maarufu zaidi ya 600 na timu 30 katika nchi 10 ndani ya mabara matatu, na kufanya kuwa mpira pekee wa adidas uliofanyiwa majaribio makubwa ili kuhakikisha unafaa kwa hali zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako