• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ivory Coast yafanya kweli kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Japan

    (GMT+08:00) 2014-06-16 14:24:34

    Miamba ya soka barani Afrika Ivory Coast (the Elephant) imefungua nyuso za waafrika baada ya kuishinda Japan kwa mabao 2-1. Ivory Coast ilijipatia mabao yake kupitia wachezaji Wilfried Bony na aliyekuwa mchezaji wa Arsenal Gervinho huku Japan ikifunga kupitia mshambuliaji wake keisuke Honda. Ushindi huo wa Ivory Coast ni wa kwanza miongoni kwa timu za bara la Afrika na unaiweka timu hiyo sawa kwa pointi na Colombia ambayo iliifunga Ugiriki mabao matatu kwa nunge. Ikiwa ni mara ya tatu kwa Ivory Coast kushiriki katika michuano ya Kombe la dunia, haijawahi kuvuka hatua ya makundi. Hatahivyo mambo yalionekana kuwa mabaya kwa kocha Sabri Lamouchi ambaye aliduwaza wengi kwa kutomchezesha aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba na kusababisha miamba hiyo kuwa nyuma kwa bao moja kabla ya mapumziko. Japan ambayo ndio mabingwa wa bara Asia walikuwa hatari katika ngome ya Ivory Coast kila walipopata mpira, na walifanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya 16 kutoka mshambuliaji wao Honda. kiungo wa kati huyo anayeichezea klabu ya A.C Milan alipata pasi safi karibu na lango la upinzani kabla ya kupiga mkwaju mkali uliomduwaza mlinda mlango wa Ivory Coast.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako