• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchambuzi wa timu ya Brazil na Croatia

    (GMT+08:00) 2014-06-16 15:30:07

    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu za Afrika zinazocheza kombe la dunia nchini Brazil, tuliizungumzia timu ya taifa ya Brazil ambayo ni nchi mwenyeji wa michuano hiyo, na tulielezea jinsi ilivyofanya vizuri katika michuano mingi tu, hadi kushinda mara tano katika michuano yote iliyoshiriki ya kombe la dunia. Lakini pia tuliwajadili wachezaji mashuhuri wa zamani na wapya ambao watashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo mfano Neymar. Sasa kuanzia leo katika kipindi tutaizungumzia timu hiyohiyo ya Brazil pamoja na Croatia ambazo jana zilivaana katika mechi ya kwanza ya ufunguzi.

    kama tulivyosema awali michuano kombe la dunia imefunguliwa rasmi jana lakini kabla ya mechi ya kwanza kuchezwa kati ya Brazil na Croatia kama kawaida yule kobe mtabiri alianza kufanya kazi yake ya kutabiri, na kwa mujibu wa utabiri alioutoa, Brazil itashinda dhidi ya Croatia kwenye mechi ya ufunguzi. Kobe huyo aliamuriwa kula kipande cha samaki kilichopo chini ya bendera ya Brazil au Croatia, au mpira ambao unaonesha sare. Lakini alichagua kipande cha samaki kilichopo chini ya bendera ya nchi mwenyeji, na kuwafanya wenyeji wawe na shauku na furaha kubwa. Mbali na kobe huyo watu mbalimbali pia waliitabiria Brazil kushinda wengine walisema itatoka kifua mbele kwa mabao 2-0. Na hatimaye kweli Brazil ilishinda kwa mabao 3-1.

    Mashindano haya ambayo yatadumu kwa mwezi mmoja yanakutanisha nchi 32. Wachambuzi wa michezo wanazipa nafasi kubwa timu nne kati ya 32 kubeba taji safari hii zikiwemo Ujerumani, Hispania Argentina na Brazil. Historia inaonesha kuwa mwenyeji hafungwi kwenye mechi ya ufunguzi ambapo huko nyuma mechi 20 za ufunguzi zimeonesha wenyeji wameshinda mara 14 na kutoka sare mara 6. lakini safari kituko cha ajabu kimetokea kwenye mechi ya ufunguzi wakati ambapo wenye wamefungua goli kwanza kabisa kwenye michuano hii kwa kujifunga wenyewe. Kituko ni pale baada ya Marcelo kujifunga mwenyewe katika dakika za mwanzo na kuifanya Croatia kuongoza.

    Hata hivyo nuru ilizidi kuwaka pale Oscar alipopigilia msumari kwa kuiongeza Brazil bao la pili, lakini hata hivyo mvuto katika uwanja wa Sao Paulo ulikuwa zaidi kwa Neymar. Labda fadhili ungeeleza kwanini iwe hivyo.

    Goli la pili la Neymar alifunga dakika 19 kabla ya kipenga cha mwisho kupulizwa, goli ambalo alilipata kwa njia ya mkwaju baada ya refarii kumuadhibu Dejan Lovren kwa kumfanyia makosa Fred ndani ya eneo la hatari. Lakini watu wengiu wamekuwa wakilalamika kuwa penalty aliyopewa apige Neymar ilikuwa na utata kwani wengine waliamini kuwa Fred alijiangusha kwa makusudi. Hata timu ya Croatia ilikasirishwa mno.

    Kwa upande wake kocha wa Croatia Niko Kovac amesema kuwa hakuna faida ya timu yake kusalia brazil haswa baada ya timu yake kuambulia kichapo cha mabao 3-1 na Brazil katika mechi ya ufunguzi. Kovac aliudhika sana na kauli ya refarii wa mechi hiyo Yuichi Nishimura ya kumwadhibu Dejan Lovren kwa kadi ya njano na kisha kuipa Brazil mkwaju wa adhabu hata baada ya kumgusa Fred katika mshikeshike ya kuwania mpira ndani ya eneo la lango la Croatia ambapo Neymar aliufuma kimiani mkwaju huo na kuiweka Brazil mbele kwa mara ya kwanza katika mechi hiyo. Lakini Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari kwa upande alimsifu refarii huyo kutoka Japan kwa kauli hiyo.

    Brazil na Croatia waliwahi kukutana katika michuano ya Ujerumani mwaka 2006 ambapo walipangwa kundi F. katika mechi waliyo Brazil pia ilitoka kifua mbele shukurani kwa Kaka ambaye aliingiza bao hilo kwa hiyo jana historia ilijirudia. Hakuna mchezaji hata mmoja wa Brazil aliyecheza mwaka huo ambaye amecheza jana, lakini kwa Croatia kuna wachezaji wawili akiwemo golkipa Stipe Pletikosa na kepten Darjio. Lakini tarehe kama hiyo ya jana Brazil pia itaikumbukasana kwani mwaka 1938 nchini Ufaransa, Brazil ilitoka sare ya 1-1 katika hatua ya robo fainali dhidi ya Czechoslovakia, hata hivyo ilibidi zikutane tena baada ya saa 48 na safari hiyo Brazil ikashinda 2-1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako