Usiku wa kuamkia juzi Jumapili Mario Balotelli aliifungia Italia bao muhimu walipoichapa England 2-1 kwenye mchezo wao wa kwanza wa fainali za Kombe la Dunia ndani ya Kundi D, baadaye alisema bao hilo ni maalumu kwa mchumba wake, mrembo Fanny Neguesha, ambaye alimvisha pete wiki iliyopita. Balotelli alifunga bao hilo kwenye dakika ya 50 na kuinyamazisha England ambayo ilikuwa na mtumaini ya kupata matokeo mazuri baada ya Daniel Sturridge kusawazisha bao la utangulizi la Italia lililofungwa na Claudio Marchisio. Straika huyo wa AC Milan alikuwa na kila kitu cha kusema kuhusu mchumba wake huyo mrembo wa Kibelgiji aliyekuwa uwanjani hapo kumshangilia mpenzi wake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |