• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yaona jua baada ya miaka 16

    (GMT+08:00) 2014-06-24 16:45:26

    Mchezaji wa Nigeria Peter Odemwingie kwa mara ya kwanza ameipatia ushindi Nigeria iliyopambana na Bosnia-Hercegovina na kuilaza kwa mabao 1-0 katika mechi yao ya pili ya kundi F katika kombe la dunia, ushindi huo wa Nigeria unamaanisha kuwa Bosnia-Hercegovina haitoendelea mbele kwenye michuano hiyo. Ushindi wa mwisho wa Super Eagles ulikuwa ni mwaka 1998. Bao hilo la pekee lilifungwa katika kipindi cha kwanza dakika ya 29 baada ya Odemwingie kupokea pasi safi kutoka kwa Emenike. Peter Odemwinge ni bao lake kwanza kufunga katika kombe la dunia baada ya miaka minne. Bao hilo hata hivyo litajadiliwa kwa upana na marefu ikizingatiwa kuwa wachezaji wa Bosnia walimlalamikia vikali refarii wa mechi hiyo wakisema kuwa Emenike alimkanyaka nahodha wa Bosnia Spahic kabla ya kumpa odemwinge pasi muruwa. Aidha msaidizi wa refarii atakumbukwa kwa kumnyima bao safi Edin Dzeko aliyesemekana kaotea lakini picha za runinga zilionesha haikuwa kweli na hivyo Bosnia wataelekea nyumbani wakijua vyema kuwa mechi hiyo ingeishia sare ya Moja kwa moja isingalikuwa msaidizi wa refarii. Nigeria sasa itakabiliana na Argentina katika mechi yao ya mwisho ya makundi. Kufuatia Ushindi huo Super Eagles ipo katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 4. Nigeria itaingia katika hatua ya mtoano kama itashinda au kutoka sare na Argentina katika mechi yao ya mwisho. Vilevile Super Eagles itafuzu iwapo Bosnia itaifunga Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako