• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ghana yatoka sare ya 2-2 dhidi ya Ujerumani

    (GMT+08:00) 2014-06-24 16:45:49

    Mchezaji wa Ghana Asamoah Gyan alifanikiwa kuifungia timu yake bao la pili na kusadia Black Stars kupata pointi yake ya kwanza katika kombe la dunia baada ya kupokea kichapo cha 2-1 dhidi ya Marekani katika mechi yao ya kwanza. Baada ya kipindi cha kwanza kuishia sare ya tasa, mshikemshike baina ya timu hizo ulizaa matunda dakika tano baada ya kipindi cha pili kuanza. Mario Gotze aliifungia Ujerumani bao la kwanza kwa kichwa katika dakika ya 51 lakini furaha yao ilizimwa kwani Andre Ayew akaisawazishia Black stars dakika tatu tu baadaye. Matumaini ya timu ya Afrika kufuzu kwa mkondo wa pili yaliimarika baada ya Nahodha Asamoah Gyan alipoiweka Ghana mbele kwenye dakika ya 63 kipindi cha pili. Hata hivyo waafrika walihuzunishwa baada ya Miroslav Klose wa Ujerumani kuisawazishia ujerumani kwenye dakika ya 71 na hivyo timu hizo zikagawana pointi baada ya mechi kukamila mabao yakiwa 2-2. Kufuatia bao hilo la Klose mjerumani huyo anayeicheza Lazio ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika historia ya kombe la dunia kwa pamoja na Ronaldo. Klose amefunga jumla ya mabao 15. Kwa upande wake Asamoa Gyan naye ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka barani Afrika ambaye amefunga mabao katika michuano mitatu ya kombe la dunia. Vijana wa Joachim Low sasa wamejikita kileleni mwa kundi G wakiwa na alama 4 moja zaidi ya Marekani huku Ghana ikiwa ya tatu na alama moja kutokana na sare hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako