• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Neymar aipeleka Brazil raundi ya timu 16

    (GMT+08:00) 2014-06-24 16:46:18

    Magoli mawili yaliyoingizwa na mchezaji wa timu ya Brazil Neymar katika mechi yao dhidi ya Cameroon, yameihakikishia nchi hiyo kufuzu hatua ya mtoano kwenye kombe la dunia. Mchezaji huyo mwenye miaka 22 alitoa ushindani mkali na kuingiza magoli katika kipindi cha kwanza, huku Fred na Fernandinho waking'ara katika kipindi cha pili na kuihakikishia nafasi katika timu 16 huku wakiwa mabingwa kwenye kundi lao A. Katika hatua hii Brazil sasa itavaana na Chile siku ya Jumamosi katika uwanja wa Belo Horizonte. Cameroon nayo ilijikaza kiume baada ya kufanya mashambulizi makali ambayo yalipelekea uwanja uliokuwa ukizizima kwa shangwe kuwa kimya wakati Matip alipofanikiwa kusawazisha goli la kwanza la Brazil katika dakika ya 26. hadi mpira unamalizika matokeo yalikuwa Brazil 4 na Cameroon wakiambulia goli moja tu la kufutia machozi. Hadi sasa timu ambazo zimeshayaaga mashindano hayo ni Cameroon Kundi A, Croatia Kundi A Australia Kundi B, Hispania Kundi B, Uingereza Kundi D na Bosnia-Hercegovina Kundi F. Kwengineko katika mechi kati ya Hispania na Australia, Hispania imeona mwezi kwa kuichabanga Australia magoli 3-0, nayo Uholanzi iliibuka washindi kwa kupata magoli 2-0 dhidi ya Chile, na katika mchezo kati ya Croatia na Mexico, Mexico walitoka kifua mbele kwa mabao 3-1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako