• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uholanzi vinara wa kundi B baada ya kuwalaza Chile, sasa kuvaana na Mexico

    (GMT+08:00) 2014-06-24 16:46:43

    Timu ya Uholanzi imemaliza ikiwa nafasi ya kwanza kwenye kundi B baada ya magoli kutoka kwa Leroy Fern na Memphis Depay kuwapa ushindi dhidi ya Chile katika mechi yao ya mwisho ya makundi iliyocharazwa huko Sao Paulo. Timu zote mbili tayari zilikuwa zimeshafuzu raundi ya pili baada ya kuanza kwa vishindo na kupata ushindi dhidi ya Hispania na Australia. Chile sasa itavaana na Brazil katika raundi ya pili, huku upande wa Louis van Gaal ukikutana na Mexico. Mechi hiyo ilikosa mshawasha huku ikiwa na faulu nyingi na hadi muda wa mapumziko timu hizo zilitoka zikiwa na sare ya tasa, hata hivyo katika dakika ya 77 kipindi cha pili, Fer alifunga kwa kichwa, kabla ya Depay kumalizia dakika ya mwisho akiingiza goli la 2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako