Mshambuliaji wa Lille ya Ufaransa, Mkenya Divorc Origi ambaye ni raia wa Ubelgiji aliyeifungia Ubeljiji bao la pekee na la ushindi dhidi ya Russia katika mechi yao ya pili ya kundi H, amesema anajivunia kuwa mkenya licha ya kuwa anaiwakilisha Ubeljiji. Bao hilo la dakika za mejeruhi kwenye mechi hiyo ndiyo lililoiwezesha Ubeljiji kufuzu raundi ya pili ya timu 16. Origi ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba baada ya kuondoka kwa Romelu Lukaku alifuma bao hilo la pekee katika dakika ya 88 kipindi cha pili, baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Eden Hazard. Origi, mwanawe Mike Okoth, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars atakua mchezaji wa kwanza wa Afrika Mashariki kuiwakilisha Ubelgiji, na yuko pamoja na wachezaji nyota kama vile Vincent Kompany wa Manchester City na Eden Hazard wa Chelsea. Origi alisema anafurahia mizizi yake na kuwa anajivunia bao hilo na familia yake iliyokuwa uwanjani kumshabikia. Pia amesema hili lilikuwa ni tukuio maalumu kwake kwa Kenya na Ubeljiji.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |