• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Uholanzi ailalamikia FIFA kwa hila zake kwenye ratiba ya kombe la dunia

    (GMT+08:00) 2014-06-24 16:47:35

    Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal amelishutumu shirikisho la soka duniani FIFA kwa kufanya hila wakati lilivyopanga ratiba ya michuano ya Kombe la Dunia. Wenyeji Brazil walicheza mechi mbili kabla ya Uholanzi kucheza, lakini watacheza tena baadaye katika mechi ya mwisho ya makundi, jambo ambalo Van Gaal anadai sio la haki. Alisema katika Kombe la Dunia taifa linaloandaa mechi hizi hupendelewa. watakaomaliza katika nafasi ya kwanza katika kundi A iliyoko Brazil watachuana na watakaomaliza katika nafasi ya pili katika kundi B siku ya Jumamosi, huku atakayemaliza katika nafasi ya pili katika kundi A akimenyana na atakayemaliza katika nafasi ya kwanza kundi B siku itakayofuata. Amesisitiza kuwa iwapo angechagua yeye, asingependa kucheza dhidi ya Brazil, ingawa Croatia na Mexico nao pia sio wapinzani dhaifu. Mkufunzi huyo anayechukua hatamu Manchester United pia aliwashutumu marefa katika mashindano hayo, ambapo alisema walitoa penalti zisizo za haki dhidi ya timu yake katika mechi mbili za ufunguzi ambazo Uholanzi waliibuka washindi dhidi ya Hispania na Australia. Katika matukio yote mawili, timu pinzani zilifunga na kuwalazimu Uholanzi kutoka nyuma na kushinda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako