Mchezaji wa Uruguay Luis Suarez anakabiliwa na sakata jingine la kumng'ata mchezaji kwa mara ya tatu sasa baada ya kudaiwa kumng'ata mchezaji wa Italia Giorgio Chilleni kwenye michuano ya kombe la dunia. Mshambuliaji huyo wa Liverpool alimrukia mlinzi wa Italy Chiellini muda mfupi tu kabla Diego Godin kupata goli la na kuifanya Uruguay kushinda kwa mabao 2-1. Baada ya kung'atwa, Chiellini alivua jezi yake na kumuonesha refarii, lakini alimpuuza na kutochukua hatua yoyote. Kama Fifa itamchukulia hatua Suarez anaweza kufungiwa mechi 24 au miaka miwili. Baada ya tukio hilo Suarez alijiangusha chini huku akiwa amekamata mdomo wake akiashiria kuwa amepigwa kiwiko cha mdomo. Suarez ambaye alikabiliwa na sakata la kukamata mpira na kuizuia Ghana kushinda mwaka 2010 katika kombe la dunia, ameiambia televisheni ya Uruguay kuwa hayo ni mambo yanayotokea kiwanjani, na ilikuwa ni wawili wao tu ndani ya eneo hilo, na kudai kuwa Chiellini alimgonga kwa bega lake. Fifa inasubiri ripoti ya refarii ili kuamua kama ichunguze tukio hilo au la. Kocha wa Italia ambaye alijiuzulu mara tu nchi yake ilipotolewa kwenye michuano hiyo alisema hajaona picha ya video ila ameona alama za kungatwa kwenye bega la Chiellini. Suarez alilazimika kukaa nje kwa mechi 10 baada ya kumng'ata kiungo wa Chelsea Branislav Ivanovic aprili 2013.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |