Ugiriki imefuzu katika raundi ya timu 16 kwenye michuano ya kombe la dunia kwa mara kwanza huku wakipata ushindi katika dakika za majeruhi. Mchezaji wa Celtic Gergio Samara alipata mkwaju katika dakika za majeruhi na kukamilisha ushindi baada ya kufanyiwa madhambi na Giovanni Sio. Ugiriki ilikuwa ikiongoza kwenye kipindi cha kwanza wakati mchezaji aliyebadilishwa Andreas Samaris kufunga kufuatia Cheik Titos kufanya makosa kwenye ulinzi. Hata hivyo mchezaji wa Ivory Coast Wilfred Bony alisawazisha goli la Samaras katika dakika ya 74 na baadaye Samaras akapata mkwaju katika dakika ya mwisho. Mara tu baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo kocha wa Ivory Coast Sabri Lamouchi alijiuzulu ukocha wa kikosi hicho. Sasa Ugiriki itavaana na Costa Rica katika raundi ya pili siku ya Jumapili huko Recife, huku Ivory Coast wakiyaaga mashindano katika hatua ya makundi kwa michuano mitatu sasa ya kombe la dunia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |