• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Ivory Coast Sabri Lamouchi ajiuzulu

    (GMT+08:00) 2014-06-25 15:20:57

    Kocha wa Ivory Coast ambaye alikuwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Sabri Lamouchi amejiuzulu kama kocha wa nchi hiyo baada ya Ivory Coast kufanya vibaya na kushindwa kufikia hatua ya mtoano kwenye kombe la dunia. The Elephant jana walishindwa 2-1 na Ugiriki katika mechi yao ya mwisho ya kundi C, ikimanisha kuwa wamemaliza wakiwa nafasi ya tatu huku wapinzani wao wakiwa nafasi ya pili. Mkataba wa Lamouchi unakamilika hadi kombe la dunia litakapotia nanga. Ivory Coast ilihitaji hata sare kuchukua nafasi ya pili na kuwawezesha kujiunga na Colombia katika raundi ya pili. Lamouchi amesema baada ya kazi ngumu na kujitolea muhanga, Waivory Coast wanahuzuni kubwa. Lamouchi ambaye ni kiungo wa zamani wa Auxerre na Monaco ambaye pia aliichezea Parma na Inter Milan. Alichaguliwa kuongoza jahazi la Ivory Coast Mei 2012 ikiwa ni kazi yake ya kwanza kuongoza. Wakati nchi hiyo ilipofikia hatua ya robo fainali kwenye kombe la mataifa ya Afrika alikuwa kocha wa timu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako