• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bosnia yakatisha matumaini ya Iran kwa kuifunga 3-1

    (GMT+08:00) 2014-06-26 16:10:14

    Matumaini ya Iran ya kufuzu raundi ya pili ya timu 16 bora katika Kombe la Dunia yalififia baada ya kushindwa na Bosnia-Hercegovina ambao tayari walikuwa wamekwisha ondolewa. Iran ingeweza kuendelea mbele raundi ya pili kwa kushinda lakini matumaini hayo yakakatishwa kabisa baada ya Edin Dzeko kuifungulia milango Bosnia katika dakika ya 23, na baada ya mapumziko Pjanic aliingiza bao la pili na kuonesha kila dalili kuwa Bosnia watanyakua ushindi kwenye mechi hiyo. Iran nayo ilifanikiwa kujikongoja na kupata bao la kufutia machozi katika dakika ya 82, lakini furaha hiyo haikudumu kwani Bosnia wakawabandika la tatu na kupata ushindi kwa mara ya kwanza tangu michuano hii ianze. Iran ilikuwa inahitaji ushindi wa aina yeyote na kuomba kuwa Nigeria iambulie kichapo ili iweze kufuzu. Kocha wa Bosnia Safet Susic alisema alifarijika na ushindi dhidi ya Iran huku Kocha wa Iran Carlos Queiroz akitania kwa kusema timu bora zaidi katika kundi haikufuzu, Bosnia ilionyesha kuwa ina wachezaji wazuri, na ni timu nzuri yenye tajriba nyingi. Alisema wachezaji wake walicheza vizuri sana, na anajivunia sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako