• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ghana yawafurusha Boateng na Muntari

    (GMT+08:00) 2014-06-27 14:32:58

    Wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng wamefurushwa kwenye kikosi hicho kilichoshiriki kombe la dunia kwa madai ya kutokuwa na nidhamu. Taarifa kutoka tovuti ya chama cha soka cha Ghana imesema wachezaji wote wawili wanasimamishwa mara moja, kwani Boateng ametoa matamshi machafu yaliyomlenga kocha Kwesi Appiah na Muntari ametimuliwa kwa kumshambulia mjumbe wa kamati kuu ya timu hiyo Moses Armah. Taarifa hiyo imekuja saa kadhaa kabla Ghana haijatolewa kwenye mashindano ya kombe la dunia. Taarifa imesema sakata linalomhusisha kiungo wa kati wa AC Milan Muntari mwenye miaka 29 lilitokea siku ya Jumanne huku lile la mchezaji wa klabu ya Schalke 04 Boateng mwenye miaka 27 likitokea siku hiyohiyo wakati timu hiyo ilipokuwa katika mazoezi katika eneo la Maceio. Hayo yote yanajiri siku moja tu baada ya serikali ya Ghana kutuma dola milioni 3 nchini Brazil ili kuwalipa wachezaji wa timu hiyo fedha zao za kushiriki katika michuano ya kombe la dunia. Awali wachezaji wa Black Stars walisusa kucheza mechi kati yake na Ureno kama hawakupewa fedha hizo swala lililoilazimu serikali kuingilia kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako