• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cameroon kufanya uchunguzi kujua sababu ya timu yake kufanya vibaya kwenye kombe la dunia

    (GMT+08:00) 2014-06-27 14:33:18

    Rais wa Cameroon Paul Biya ametaka ufanyike uchunguzi wa kina kutokana na nchi hiyo kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la dunia. Kampeni za The Indomitable Lions nchini Brazil zilikuwa majanga kwani wameshindwa mechi zote tatu za makundi, wachezaji kutolewa na wengine kugombana kiwanjani wakati wa mechi. Cameroon imefungwa magoli 9 na kupata goli 1 tu na imekuwa timu ya kwanza kufungashwa virago kwenye michuano hiyo mikubwa. Waziri mkuu Philemon Yang naye ameamuru ufanywe uchunguzi ili kujua sababu ya yote hayo. Juu ya hayo Alex Song alioneshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko kwa nguvu mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic kosa ambalo limepelekea kufungiwa mechi tatu na Fifa. Kwa mujibu wa taarifa waziri mkuu atatoa matokeo ya uchunguzi ndani ya mwezi mmoja na kutoa mapendekezo ya kuijenga tena timuya taifa ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako