• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ureno yaondoka kwenye kombe la dunia na zawadi ya ushindi

    (GMT+08:00) 2014-06-27 14:33:40

    Timu ya Ureno imeondoka kifua mbele baada ya kuilaza Black Stars ya Ghana kwa mabao 2-1 katika mechi ya mwisho ya makundi. Bao la ushindi la Ureno lilifungwa na Cristiano Ronaldo, hata hivyo Ureno ilikuwa imeshatolewa nje ya michuano hiyo baada ya kushindwa mechi zao za kwanza. Ghana itajilaumu kwa kushindwa kupata ushindi uliohitajika kuihakikishia nafasi katika 16 bora baada ya John Boye alipojifunga mwenyewe. Asamoah Gyan alifunga bao la kuisawazishia Black stars lakini haikutosha kuifufua kampeni yao kwani walihitaji ushindi wa aina yeyote na kuomba kuwa Ujerumani iishinde Marekani ili waweze kufuzu kama washindi wa pili katika kundi G. Ronaldo hata hivyo atamshukuru kipa wa Ghana Fatawu Dauda kwa sifa alizopata baada ya kufunga bao la ushindi kufuatia kipa huyo kumzawadia mpira katika eneo la lango naye akaifuma kimiani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako