• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria na Algeria zatolewa nje ya kombe la dunia

    (GMT+08:00) 2014-07-01 16:30:39

    Ujerumani imefanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali baada ya kuwalaza mbweha wa Jangwani Algeria kwa mabao 2-1 katika kipindi cha ziada. Sasa itavaana na Ufaransa iliyowatoa wanigeria. Katika vipindi vyote viwili vya muda wa kawaida timu hizo zilishindwa kutambiana, na baada ya muda wa ziada kuanza tu Ujerumani ilianza kuonesha hasira zake katika dakika ya 92 kwa kupachika bao la kwanza. Algeria ilishindwa kujibu ndipo katika ya 119 Ujerumani wakaamua kuwafunga midomo kabisa mbweha hao wa jangwani wasije wakatafuna kwa kuwapigilia bao la pili, hata hivyo dakika moja baadaye Algeria ilicharukwa kwa uchungu na kuamua kuingiza bao lake la kwanza. Lakini juhudi zao hazikuzaa matunda na kuhitimisha mchezo wakiwa nyuma kwa bao 1, kwa matokeo hayo sasa Afrika haina tena nchi inayoiwakilisha kwenye michuano hiyo baada ya Nigeria nayo kuondolewa na Ufaransa katika mechi iliyochezwa huko Brasilia. Ufaransa iliingiza magoli mawili katika dakika 11 za mwisho huku Nigeria ambayo ilimiliki mpira kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha pili ikiwa kimya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako