Timu ya Ugiriki imeamua kukataa kupokea malimbikizi ya marupurupu yao kutoka serikalini. Timu hiyo iliyoondolewa na Costa Rica katika hatua ya mtoano ilimwandikia waziri mkuu wa Ugiriki Antonis Samaras barua ikimtaka atumie fedha hizo kujenga uwanja mpya wa soka utakaotumika kutambua na kukuza vizazi vipya vya soka. Bwana Samaras aliahidi kutekeleza ombi la wachezaji wake alipozungumza kwa njia ya simu na maafisa wa chama cha soka cha Ugiriki. Timu hiyo iliambulia kichapo cha mabao 5-3 kupitia mikwaju ya penalti mikononi mwa Costa Rica. Na katika kufurahia ushindi huo mashabiki na raia wa Costa Rica walimiminika barabarani juzi kushangilia ushindi wa kihistoria wa timu yao iliyofanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwenye Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza. Mashabiki katika mji mkuu wa Costa Rica, San Jose, walikusanyika katika eneo la Fuente de la Hispanidad, ambalo hutumika kwa ajili ya sherehe za kitamaduni, wakiwa na bendera za taifa lao, nywele bandia na jezi zao wakiishangilia timu yao kwa ushindi huo. Shabiki mmoja ambaye ni mhudumu wa mgahawa, Teo Prestinary (43), katika fukwe za Nosara, alisikika akisema Taifa limeanguka. Kunaweza kukatokea tetemeko la ardhi. Costa Rica ilifikia hatua ya kuitoa Ugiriki baada ya kuzichapa Uruguay na Italia na kulazimisha sare na England, wakati ilitabiriwa kuwa ndiyo timu dhaifu katika kundi lao
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |