• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa michezo wa Nigeria asema Keshi hajajiuzulu ukocha

    (GMT+08:00) 2014-07-04 10:23:26

    Baada ya Nigeria kufungwa magoli 2-0 na Ufaransa kwenye michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko nchini Brazil na kupeleka kuondolewa kwenye michuano hiyo, Keshi alisema mechi hiyo itakuwa ya mwisho kwake akiwa na timu hiyo, taarifa ambayo baadhi ya vyombo vya habari viliitafsiri vibaya. Kwenye taarifa iliyosainiwa huko Abuja na msaidizi wake maalumu wa mambo ya habari Patrick Omorodion, waziri wa michezo nchini Nigeria amesema si sahihi kwamba Keshi amejiuzulu, na kwamba alimueleza kuwa hakusema hivyo, ila tu mkataba wake unamalizika. Kwa mujibu wa waziri, Keshi anapaswa kuheshimiwa na chama cha soka cha Nigeria ambao walitakiwa kwanza waongee nae kuhusu mkataba wake kuliko kulitangaza kwenye vyombo vya habari. Wakati huohuo, Keshi naye pia amekanusha uvum kuhusu yeye kujiuzulu, na kusisitiza kuwa aliwaambia wachezaji tu kwamba mechi dhidi ya Ufaransa huenda ikawa ya mwisho kwake na timu hiyo kwani mkataba wake unamalizika wakimaliza tu michuano ya kombe la dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako