Wachezaji saba wa Ujerumani, wanaugua mafua, saa 24 tu kabla ya mechi yao ya robo fainali katika kombe la dunia dhidi ya Ufaransa. Hata hivyo kocha Joachim Low hakutaja majina ya wachezaji wagonjwa isipokuwa alisema theluthi moja ya wachezaji wanaumwa na koo ila wote wameweza kufanya mazoezi. Mats Hummels na Christoph Kramer waliugua mapema wiki hii huku Mat akikosa mechi ya mtoano dhidi ya Algeria Jumatatu. Low anaamini kuwa safari za hapa na pale nchini Brazil na tofauti ya mazingira kwa mechi zao nne hadi sasa pamoja na joto kali na mvua kubwa pia hali ya ubaridi huko Porto Alegre, ndio sababu ya wachezaji wake kuugua. Lakini aliongeza kuwa, hali sio mbaya sana, na hataki watu wadhani kuwa wanakabiliwa na wakati mgumu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |