Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter ameyasifu mataifa madogo kwa kuyaadhibu mataifa ''makubwa' 'kisoka. Blatter aliyasema hayo baada ya kubainika kuwa mataifa yote yaliyochukua nafasi ya kwanza katika makundi yao na kuingia hatua ya mtoano ndiyo yaliyofuzu kucheza robo fainali. Hii pia ilitoa sura mpya kwani timu 4 za bara Ulaya zilifuzu katika hatua ya robo fainali sawa na 4 kutoka mataifa ya Amerika kusini kinyume na matarajio ya wengi hasa baada ya kushuhudia mataifa yenye sifa kubwa katika kombe la dunia wakiwemo mabingwa watetezi wa dunia Hispania, mabingwa wa zamani Uingereza na Italia wakitolewa nje ya michuano hiyo mapema katika raundi ya kwanza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |