Nyota wa Pop wa Colombia Shakira anatazamiwa kutumbuiza katika sherehe ya ufungaji wa kombe la dunia, itakayofanyika tarehe 13 Julai kabla ya mechi ya fainali huko Reo de Jeneiro. Nyota huyo ataimba wimbo wa La La La (Brazil 2014) katika uwanja wa Maracana. Hii ni mara ya tatu mfululizo kutumbuiza kwenye sherehe za ufungaji wa kombe la dunia, baada ya kutumbuiza nchini Afrika Kusini mwaka 2010 ambapo aliimba wimbo rasmi wakawaka ( This Time for Africa) ambao umeripotiwa kuwa ni wimbo wa kombe la dunia uliopata mauzo makubwa kuliko nyimbo zote hadi sasa, na pia alitumbuiza Ujerumani mwaka 2006. Shakira ambaye timu yake ya nyumbani itavaana na Brazil katika robo fainali amesema anafurahia mno kutumbuiza siku hiyo. Sherehe hizo nchini Brazil ambazo zinahitimisha kipindi cha mwezi mzima cha soka, pia zitamshirikisha Carlos Santana na nyota wa Hip Hop Wyclife Jean ambao wataimba wimbo wa taifa pamoja na Alexandre Pires.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |