• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha Colombia chapata makaribisho makubwa nyumbani

    (GMT+08:00) 2014-07-08 11:18:02

    Maelfu ya mashabiki wamejitokeza huko Bogota nchini Colombia kuwakaribisha nyumbani wachezaji wa Colombia baada ya kufanya vizuri katika fainali za kombe la dunia. Kocha Jose Pekerman amekiongoza kikosi chake kufikia robo fainali kwa mara ya kwanza kabla ya kutolewa na wenyeji Brazil kwa mabao 2-1. Mchezaji James Rodriguez amefunga magoli 6 kwenye michuano hiyo na hadi sasa amebakia kuwa mfungaji mwenye magoli mengi zaidi kabla ya mechi za nusu fainali na amefunga katika mechi zote tano walizocheza nchini Brazil. Jumla ya magoli hayo aliyofunga kiungo huyo wa Monaco, ni pamoja na walipocheza dhidi ya Uruguay katika hatua ya mtoano ambapo Colombia ilitoka kifua mbele kwa magoli 2-0. Pia ameingiza katika mechi zote za kundi lake C walipocheza na Ugiriki, Ivory Coast na Japan. Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ametuma ujumbe akiwashukuru kwa kupeleka furaha nchini humo na kuifundisha nchi kutimiza ndoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako