• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka labadilisha maisha ya watoto wa mtaani nchini Brazil

    (GMT+08:00) 2014-07-08 19:22:15

     

    Wakati kombe la dunia la Brazil linapopamba moto na kuingia nusu fainali, mbali na kufuatilia matokeo ya mechi, tuangalie jinsi soka linavyobadilisha maisha ya watu hasa watoto katika nchi hiyo inayojulikana kwa soka.

    Tokea mwaka 2010, kabla ya kombe la dunia kufanyika, Brazil huandaa kombe la dunia la watoto wa mitaani. Mwaka huu, Claudia mwenye umri wa miaka 17 aliongoza timu yake kunyakua kombe hilo.

    "watoto wengi wanaoshiriki mechi hizi wana historia zinazotia huruma, kwa mfano, mvulana kutoka timu ya Msumbiji, alilazimika kuwa mtoto wa mitaani kutokana na ugomvi wa kila siku kati ya wazazi wake, baadaye akachukuliwa na kituo cha kuwalea watoto wa mitaani, akachaguliwa kuichezea timu ya taifa ya vijana, na sasa amerudi tena nyumbani kwao na anaendelea na maisha ya kawaida."

    Claudia anaona kuwa soka limewaletea watoto wengi nchini Brazil mafanikio na matumaini.

    "Naweza kusema soka imebadilisha sura ya maisha yangu. Ninapocheza soka, ninasikiliza mapendekezo niliyopewa na wachezaji wengine, ninajifunza kushirikiana na wenzangu, na kusahau matatizo yangu. Soka imenipa furaha."

    Mchezaji wa timu ya taifa la Brazila katika kombe la dunia la mwaka huu Neymar da Silva Santos Junior alikuwa mtoto wa mtaani. Maisha yake yalibadilika kutokana na soka, na sasa anatumia kipaji chake katika uwanja wa soka kuwasaidia wengine, ikiwemo kufadhili uwanja wa soka katika maskani yake. Msimamizi wa mradi huo anasema:

    "Sehemu hii ni muhimu kwa Neymar, sababu kila mtoto anayelelewa hapa ana historia isiyosahaulika, Neymar ni mmojawapo. Alipoteza marafiki wengi kutokana na vurugu na matumizi ya dawa za kulevya, kwa hiyo baada ya kupata umaarufu, aliamua kufadhili uwanja huu wa soka, kwa sababu alikuwa mtoto mwenye ndoto ya kucheza kwenye uwanja kama huu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako